Rais Museveni kuwania urais mwaka 2026

0
140

Chama tawala cha National Resistance Movement (NRM) cha nchini Uganda kimethibitisha Rais Yoweri Museveni kuwania tena urais katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika mwezi Januari, mwakani.

Museveni mwenye umri wa miaka 80, amekuwa madarakani tangu 1986, na ni miongoni mwa viongozi waliokaa muda mrefu zaidi madarakani barani Afrika.

Katika video iliyochapishwa na Shirika la Utangazaji la UBC kwenye mtandao wa kijamii wa X, mwenyekiti wa baraza la uchaguzi la chama tawala, Tanga Odoi amesema Museveni atachukua fomu Juni 28 kuwakilisha chama katika uchaguzi huo.

Send this to a friend