Rais Ndayishimiye: Rwanda inapanga kuishambulia Burundi

0
4

Rais wa Burundi, Évariste Ndayishimiye amesema anayo taarifa za kiintelijensia zinazoonesha kuwa Rwanda inakusudia kushambulia nchi yake.

Aidha, ametaja jaribio la mapinduzi alilosema Rwanda ilijaribu kuanzisha miaka kumi iliyopita, akilinganisha hali hiyo na kinachoendelea sasa nchini DR Congo.

Rwanda imejibu kwa kusema madai ya Rais Ndayishimiye ni ya kushangaza, na kusisitiza kwamba nchi hizo mbili zinaendelea kushirikiana kutafuta mikakati ya kulinda mipaka yao ya pamoja, ambayo imefungwa kwa zaidi ya mwaka mmoja.

Angola yajiondoa kama mpatanishi wa mzozo wa DRC

Ingawa kuna ushahidi wa Umoja wa Mataifa unaoonesha madai ya Rwanda kusaidia kikundi cha waasi cha M23 kilichochukua sehemu kubwa ya mashariki ya DRC pamoja na wanajeshi wa Rwanda, Rwanda imekanusha kuhusika na waasi hao.

Aidha, Rwanda imekana kuwa na uhusiano na kundi la waasi la Red Tabara, ambalo Rais Ndayishimiye amesema ni jeshi la kulipwa linaloungwa mkono na Rwanda kwa lengo la kutikisa utulivu wa Burundi.

Send this to a friend