Rais Ramaphosa achaguliwa kuingoza ANC licha ya kashfa zinazomkabili

0
39

Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa amechaguliwa tena kwa shangwe kuwa kiongozi mkuu wa Chama cha African National Congress (ANC) na licha ya kashfa zinazomkabili.

Rais Ramaphosa amemshinda mpinzani wake, Zweli Mkhize kwa kura 2,476 dhidi ya 1,897 ambaye pia amekuwa akishutumiwa kwa ufisadi, lakini wote wamekuwa wakikanusha madai hayo.

Kwa mujibu wa taarifa ushindi alioupata unamuweka katika nafasi nzuri ya kuongoza ANC katika uchaguzi wa mwaka 2024.

Treni za umeme kuendeshwa kwa umeme wa TANESCO

Lakini bado yuko hatarini kwani anachunguzwa na polisi, ofisi ya ushuru na benki kuu kuhusu madai kwamba alificha takribani $580,000 (TZS bilioni 1.3) kwenye sofa katika shamba lake la binafsi.

Jopo la wataalamu wa sheria walioteuliwa na spika wa bunge limesema kuwa ana kesi ya kujibu kwani huenda alikiuka katiba na kuvunja sheria za kupambana na rushwa.

Send this to a friend