Rais Ramaphosa anusurika kuondolewa madarakani

0
43

Wabunge wa Afrika Kusini wamepiga kura kupinga ripoti ambayo inaweza kumwondoa madarakani Rais Cyril Ramaphosa na karibu wanachama wote wa chama tawala cha African National Congress (ANC) wamemkingia kifua kiongozi wao.

Katika kura zilizopigwa, kura za kuunga mkono Rais Ramaphosa kuondoka madarakani zilikuwa 148 huku jumla ya kura 214 zikimkingia kifua.

Rais alishutumiwa kwa kuficha kiasi kikubwa cha fedha za kigeni kutoka shambani mwake mwaka 2020 na baadhi zikiwa zimefichwa kwenye sofa, lakini Rais huyo ambaye anawania kuchaguliwa tena kama kiongozi wa ANC, amekanusha makosa hayo yote.

Ufafanuzi wa Waziri wa Fedha, Dkt. mwigulu Nchemba kuhusu deni la Taifa Tanzania

Mjadala kabla ya upigaji kura ulilenga ripoti huru ambayo ilihitimisha kuwa huenda alikiuka katiba.

Aidha, Chama cha ANC kiliwaambia wabunge wake kuzuia uwezekano wa kufunguliwa mashtaka, ingawa wachache walivunja safu na kuungana na vyama vya upinzani kukubali ripoti hiyo na kuruhusu kesi za kumshtaki zianze.

Kwa vile sasa Rais Ramaphosa amenusurika kwenye kura hiyo, anafikiriwa kuwa anaweza kushinda tena katika kongamano la chama chake ambalo litaanza Ijumaa. Kisha atakuwa katika nafasi nzuri ya kuwa mgombea urais wa ANC katika uchaguzi ujao wa 2024.

Send this to a friend