Rais Ramaphosa atangaza tatizo la umeme kuwa janga la kitaifa

0
46

Kutokana na tatizo kubwa la kukatika kwa umeme linaloikumba Afrika Kusini, Rais Cyril Ramaphosa ametangaza kuwa tatizo hilo ni janga la kitaifa linaloiletea tishio taifa hilo lililoendelea kiviwanda barani Afrika.

Akizungumza katika hotuba yake ya kila mwaka aliyoitoa bungeni Februari 9, 2023, Ramaphosa amekiri kuwa taifa liko kwenye mzozo mkubwa wa kinishati huku akiulaumu zaidi ufisadi.

Katika hotuba hiyo wabunge wa chama cha Economic Freedom Fighters (EFF) walimpinga vikali Rais Ramaphosa huku wakimzuia kuhutubia kwa madai kuwa hana haki hiyo na wengine wakijaribu kupanda jukwaani kufanya fujo.

Kwa mujibu wa Reuters, Ramaphosa aliweka wazi kwamba uhaba wa umeme umekuwa ukiendelea kwa miaka mingi, ikiwa ni matokeo ya ucheleweshaji wa ujenzi wa vituo vipya vya nishati ya makaa ya mawe.

Spika Tulia aagiza kauli ya Waziri Mwigulu ifutwe

“Mgogoro umeendelea kubadilika na kuathiri kila sehemu ya jamii. Ni lazima tuchukue hatua ili kupunguza athari za mgogoro huo kwa wakulima, kwa wafanyabiashara wadogo, kwenye miundombinu yetu ya maji na mtandao wetu wa usafiri,” amesema Ramaphosa.

Inaelezwa kuwa kukatika kwa umeme nchini humo kunatarajiwa kupunguza ukuaji wa uchumi katika taifa hilo hadi asilimia 0.3 tu kwa mwaka huu.

Send this to a friend