Rais Ruto akataa pendekezo la kuongeza mshahara wake

0
26

Rais William Ruto ametupilia mbali pendekezo la hivi karibu lililotolewa na Tume ya Mishahara na Marupurupu (SRC) kuhusu kuongezewa mishahara kwa maafisa wakuu Serikalini.

Ruto amepuuza pendekezo la nyongeza ya mishahara kwa Rais, Naibu Rais, Makatibu wa Baraza la Mawaziri, wabunge na miongoni mwa maafisa wengine wakuu, badala yake ameiagiza SRC kubuni mbinu za kusawazisha mishahara kwa maafisa wa serikali ili kuendana na viwango vya kimataifa.

“Kwa maafisa wengine wa Serikali, mimi, naibu wangu, mawaziri, na wale wadosi wengine wa Bunge, sisi mambo yetu tungojee tafadhali. Hiyo mishahara itakwama hapo.

Waziri Mkuu: Tumemtoa TICTS tunamuweka DP World, hakuna geni

Nimeiagiza SRC itupe kanuni bora za kimataifa kwa sababu tunahitaji kupunguza pengo kati yetu sote tunaofanyia kazi watu wa Kenya. Tunapaswa kuhakikisha kuwa pengo kati ya mtu anayelipwa kidogo zaidi na yule alilipa pesa nyingi sio kubwa sana kwa sababu sisi sote ni wafanyakazi,” amesema.

Ameongeza “Haiwezekani watu walio juu wanapata zaidi ya watu wa chini mara 100, si sawa kwa sababu tunaishi nchi moja, tunanunua chakula kimoja, tunaenda duka moja.”

Send this to a friend