Rais Ruto alaani walioshambulia polisi wakati wa maandamano

0
94

Rais wa Kenya, William Ruto amelaani mashambulizi dhidi ya polisi yaliyotokea wakati wa maandamano ya kizazi cha Gen-Z siku ya Jumatano, akisema hali hiyo inahatarisha utulivu wa taifa.

Ruto amesema serikali yake itaendelea kuwaunga mkono na kuwalinda maafisa wa usalama ili waweze kutekeleza majukumu yao, akisisitiza kuwa usalama wa taifa unaweza tu kupatikana kwa kuwaunga mkono maafisa hao.

“Hatuwezi kuwa na nchi ambako wahalifu wanawakimbiza polisi wetu. Kama maisha ya polisi yako hatarini, familia zetu ziko salama vipi? Hali hii lazima ibadilike,” amesema Rais Ruto.

Ameongeza, “Tutasimama na kila mwanamume na mwanamke aliye kwenye sare, na kuwalinda wanapotekeleza kazi yao. Hivyo ndivyo tutapata Kenya iliyo salama na thabiti, ambako maendeleo yanaweza kufanyika.”

Send this to a friend