Rais Ruto apunguza ulinzi wa Kenyatta na wanafamilia wake

0
46

Ripoti mbalimbali nchini Kenya zimeeleza kuwa baadhi ya mabadiliko yamefanywa katika timu ya ulinzi ya Rais Mstaafu wa Kenya, Uhuru Kenyatta miezi michache tangu akabidhi urais kwa naibu wake wa zamani, William Ruto.

Maagizo hayo yanaripotiwa kutekelezwa siku ya Alhamisi Februari 2, 2023 yakiwataka maafisa wa kitengo cha GSU na baadhi kutoka kitengo cha kumlinda Rais kuondoka katika vituo vyao na kuripoti katika makao makuu.

Kampuni ya Adani yakanusha ripoti iliyotolewa na Marekani

Mabadiliko hayo pia yanasemekana kuwa ni kupunguzwa kwa idadi ya maafisa usalama wanaolinda nyumba za baadhi ya wanafamilia wa Kenyatta akiwemo mama yake, Mama Ngina.

“Kutoka maafisa 96 wa ngazi ya juu aliokuwa nao ameachiwa maafisa 25, huku mke wa Rais huyo wa zamani akiwa na watano,” chanzo kiliambia tovuti ya Nation hapo jana.

Send this to a friend