Rais Ruto awaongeza mishahara maafisa polisi na magereza

0
71

Rais wa Kenya, William Ruto ametangaza kuwa nyongeza ya mishahara kwa maafisa wa polisi, magereza na maafisa wengine wa mashirika ya usalama itaanza kutekelezwa mwezi huu.

Ameyasema hayo katika Ikulu ya Nairobi wakati wa kuapishwa kwa Kamishna Jenerali mpya wa Jeshi la Magereza, Patrick Aranduh Mwiti, ambapo ameeleza kuwa nyongeza hiyo ni ahadi aliyoiahidi mwishoni mwa mwaka jana.

“Kama ahadi niliyotoa kwa wanaume wetu waliovalia sare kuanzia mwezi huu tutakuwa tukitimiza ahadi yetu ya kuongeza mishahara ya maafisa wetu wa polisi, maafisa wetu wa magereza kulingana na ahadi yetu tuliyojitolea,” ameeleza.

Rais Ruto aliahidi nyongeza ya asilimia 40 ya mishahara ya maafisa wa polisi kama sehemu ya mapendekezo ya jopokazi kuhusu mageuzi ya polisi inayoongozwa na aliyekuwa Jaji Mkuu David Maraga.

Hata hivyo, Mnamo Februari mwaka huu, Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya Ndani, Raymond Omollo alithibitisha kwamba nyongeza ya mishahara itaanza Julai mwaka huu na kutekelezwa hatua kwa hatua katika miaka mitatu ijayo.

Send this to a friend