Rais Samia aagiza Serikali kusimamia misiba ya watu 17 waliofariki Tanga

0
14

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa maagizo kuwa Serikali isimamie msiba wa watu 17 waliofariki kwenye ajali mkoani Tanga hadi utakapomalizika.

Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Omary Mgumba amesema hadi kufikia sasa majeneza 16 yamekamilika na kubaki majeneza mawili ambayo mafundi wanaendelea nayo ikiwemo la Atanas Mrema ambaye alikuwa anasafirishwa kwenda kuzikwa mkoani Kilimanjaro baada ya jeneza lililokuwa limebeba mwili huo kupasuka.

Aidha, RC Mgumba amesema kuwa tayari magari mawili yamekwishapatikana kwa ajili ya kusafirisha miili hiyo ambapo kwa sasa wanasubiri maelekezo kutoka kwa familia.

Watumishi Tanga wasimamishwa kazi kwa kuchelewa kufika eneo la ajali

“Tuliwapa pumziko kidogo familia kwa sababu wana mambo mawili kuna maiti zipo mochwari na kuna majeruhi wako hospitali, kwa hiyo tulitaka utulivu wao, sasa hivi tunaenda kukaa nao ili tuone kwa pamoja kama wapo tayari kusafiri leo au wapo tayari kusafiri kesho,” amesema RC Mgumba.

Send this to a friend