Rais Samia aagiza stahiki za Hayati Dkt. Magufuli kutimizwa

0
60

Rais Samia Suluhu Hassan amemuagiza Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Mohamed Mchengerwa kuanza maandalizi ya kutimiza haki zote anazostahili aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hayati Dkt. John Pombe Magufuli.

Rais ametoa agizo hil leo wakati akimkabidhi nyumba ya kuishi Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete iliyojengwa katika Wilaya ya Kinondoni mkoani Dar es Salaam.

Kwa upande wake Waziri Mchengerwa amesema nyumba hiyo ni ya 3 kukabidhiwa ikitanguliwa na nyumba ya Rais Mstaafu Hayati Benjamin William Mkapa na Rais Mstaafu, Dkt. Ali Hassan Mwinyi na kwamba nyumba ya Baba wa Taifa, Hayati Mw. Julius Kambarage Nyerere ilijengwa na kukabidhiwa kwake na Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ).

Katika shukrani zake, Dkt. Kikwete ameishukuru Serikali kwa kutekeleza takwa hilo la kisheria, ameishukuru TBA kwa kukamilisha ujenzi tangu ulipoanza mwaka 2018 na amemshukuru Rais Samia kwa kumkabidhi nyumba hiyo.

Send this to a friend