Rais Samia aagiza taasisi tano kuchunguzwa

0
27

Rais Samia Suluhu ameiagiza Tume ya Kuangalia jinsi ya Kuboresha Taasisi za Haki Jinai nchini kuichunguza Jeshi la Polisi, Ofisi ya Taifa ya Mashitaka, Jeshi la Magereza na Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa lengo la kufanya maboresho ya kina ili kukidhi matakwa ya Serikali na jamii kwa ujumla.

Agizo hilo limetolewa leo Januari 31, 2023 Ikulu Chamwino jijini Dodoma wakati wa uzinduzi wa tume hiyo yenye wajumbe 11 inayoongozwa na Jaji Mkuu Mstaafu, Mohamed Othman Chande pamoja na Makamu Mwenyekiti, Balozi Ombeni Sefue.

Tume hiyo ambayo itafanya uchunguzi kwa kipindi cha miezi minne kuanzia Februari 1 hadi Mei 30 mwaka huu imeagizwa pia kuichunguza Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) ili kubaini endapo taasisi hiyo inazuia na kupambana na rushwa au wakati mwingine inahamashisha rushwa.

Watumishi wasioenda likizo wanaiibia Serikali

Aidha, Rais Samia amesema kumekuwa na kesi kadhaa za kuwatia hatiani raia wasiokuwa na hatia kwa tuhuma za dawa za kulevya huku uhalifu huo ukifanywa na baadhi ya askari wenyewe.

“Jeshi la Magereza na Mamlaka ya kudhibiti na kupambana na dawa za kulevya, tumekuwa na kesi kadhaa, vijana wetu hawa wanakwenda kumtegeshea mtu halafu wanakwenda wanazunguka unaona kikundi cha watu hicho hapo, tumekuja kukukagua kukagua madawa ya kulevya kumbe wamezitegesha wenyewe, wanatia hatiani watu wasiopaswa kutiwa hatiani,” ameeleza Rais Samia.

Mbali na hayo, Rais Samia ameiagiza tume kuangalia matumizi ya TEHAMA, ubunifu na upandishwaji wa vyeo pamoja na malalamiko ya wafanyakazi katika taasisi hizo.

Send this to a friend