Rais Samia aahidi kuiunganisha zaidi Tanzania na nchi za Afrika Mashariki

0
35

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania inaendelea na utekelezaji wa miradi mbalimbali ya barabara zitakazoiunganisha na nchi za Afrika Mashariki pamoja na nje ya Afrika Mashariki.

Amesema hayo wakati wa hafla ya ufunguzi wa sehemu ya kwanza (Sakina Tengeru – 14km) ya barabara ya Afrika Mashariki (117km) na Arusha Bypass (42.4km), jijini Arusha na kuhudhuriwa na viongozi mbalimbali akiwemo Rais wa Kenya, Uhuru Kenyatta.

China yabadili masharti ya visa kwa wasafiri wa Tanzania

Amesema Serikali inatekeleza mradi wa reli ya kasi (SGR) itakayoiunganisha na nchi ya Burundi, Rwanda na hatimaye DR Congo, Pia inafanya jitihada za kukuza usafiri kupitia njia ya bahari na maziwa ikiwemo kuimarisha ujenzi wa bandari katika ziwa Victoria na Tanganyika pamoja na kujenga meli zitakazofanya kazi baina ya nchi za Afrika Mashariki.

Kwa upande wake Rais Uhuru Kenyatta amewasihi wananchi wa Afrika Mashariki kuwaunga mkono viongozi wao na kushirikiana ili kutekeleza miradi ya kimaendeleo itakayoinua nchi hizo na kuheshimika duniani.

“Tunaweza kubadilisha nchi zetu ziwe nchi ambazo zitakuwa viongozi, sio tu katika Afrika, lakini kwa dunia nzima, na tuheshimiwe na dunia na nchi hata za huko nje, kwa sababu ya umoja wetu na maendeleo ambayo tunaweza kutekeleza kwa sababu ya huo umoja,” amesema Rais Kenyatta.

Send this to a friend