Rais Samia aahidi kutoa milioni 10 kwa kila goli Taifa Stars

0
63

Rais Samia Suluhu Hassan ameahidi kutoa TZS milioni 10 kwa kila goli litakalofungwa na timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars) kuanzia mechi zijazo Machi 28 mwaka huu.

Akitoa taarifa hiyo baada ya ushindi wa goli 1-0 dhidi ya Uganda uliochezwa nchini Misri, Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa amesema Rais Samia Suluhu amefurahishwa sana na ushindi huo, pia amewapongeza wachezaji, benchi la ufundi, TFF na wadau wote walioshiriki katika maandalizi ya timu hiyo.

“Mheshimiwa Rais katika kuwatia ari wachezaji, katika kuwahamasisha ameamua kutoa donge nono la shilingi milioni 10 kwa kila goli ambalo Taifa Stars watalifunga kuanzia mechi zinazofuata yaani kuanzia tarehe 28 ya mwezi huu wa tatu na kuendelea mechi zingine mpaka tutakapofuzu Kwenda kucheza AFCON,” amesema Msigwa.

Ameongeza kuwa Rais Samia Suluhu anahitaji Taifa Stars kuendelea kufanya vizuri zaidi katika mchezo wa marudiano utakaofanyika Machi 28 mwaka huu mkoani Dar es Salaam.

Send this to a friend