Rais Samia aanza kurekodi kipindi cha kutangaza utalii

0
35

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameanza kurekodi kipindi maarufu cha Royal Tour chenye lengo la kuitangaza Tanzania kimataifa.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa kamati ya Rais ya kuratibu mpango wa kuitangaza Tanzania kimataifa, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Hassan Abbasi, amesema Rais Samia atatembelea na kuonesha kwa wageni hao vivutio mbalimbali vya utalii, uwekezaji, sanaa na utamaduni vilivyopo nchini. 

Rais Samia na wageni hao wa Royal Tour wameanza zoezi hilo la kurekodi maeneo mbalimbali ya vivutio vya utalii na uwekezaji Agosti 28, 2021 katika maeneo ya visiwa vya Zanzibar.

Send this to a friend