Rais Samia abadili upatikanaji huduma za afya Idodi

0
40

Rais Samia Suluhu Hassan ameboresha kituo cha afya katika Kata ya Idodi mkoani Iringa na hivyo kuwezesha wananchi wa kata mbili zinazokadiriwa kuwa na wananchi 14,630 kupata huduma za afya za uhakika.

Kituo cha afya Idodi kinatoa huduma zote muhimu ikiwemo huduma za upasuaji, uongezaji wa damu na huduma za uzazi ambao awali wananchi walilazimika kuzifuata mbali jambo ambalo lilihatarisha maisha ya wagonjwa kutokana na changamoto za barabara na umbali wa kufika hospitalini.

Erasto Mapunda, dereva wa gari la kubebea wagonjwa wa dharura anasema kuna muda ilimchukua siku mbili mfululizo akiwa kuendesha gari bila kupumzika akiwahamisha wagonjwa kutoka kata hiyo na kuwapelekwa hospitali kubwa ambako wangeweza kupatiwa matibabu.

Wakazi wa Idodi wametoa shukrani zao kwa Rais Samia kwa kuwezesha upatikanaji huduma za afya bora karibu na makazi ya wananchi, huku Mganga Mfawidhi wa kituo hiko, Dkt. Frank Kitumbika akisema kwa sasa wanaweza kufanya upasuaji kwa urahisi.

Send this to a friend