Rais Samia afanya mabadiliko Baraza la Mawaziri

0
13

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mabadiliko madogo ya Baraza la Mawaziri ambapo amemteua Dkt. Stergomena Lawrence Tax kuwa Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki. Awali Mhe.

Dkt. Tax ambaye alikuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa anachukua nafasi ya Balozi Liberata Mulamula.

Pia, amemteua Innocent Lugha Bashungwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa.

Awali alikuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Katika hatua nyingine Rais amemteua Angellah Jasmine Kairuki kuwa Mbunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

Pia amemteua kuwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI).

Send this to a friend