Rais Samia afanya uteuzi Shirika la Petroli TPDC

0
60

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mkurugenzi Mtendaji Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania  (TPDC), Mussa  Makame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri na Uwekezaji wa Mfuko wa Mafuta  na Gesi (Portfolio Investment Advisory Board).

Aidha, Rais Samia  amewateua wajumbe wanne wa bodi hiyo akiwemo Dkt. Suleiman Missango, Meneja Msaidizi Kurugenzi ya Utafiti na Sera, Benki Kuu ya Tanzania (BOT).

Afisa Fedha Mwandamizi kutoka Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC), Safiel Msovu.

Mwingine ni Mkurugenzi wa Kampuni ya Express Microfinance company Ltd, Shogholo Msangi na aliyekuwa  Mhasibu Mkuu wa Serikali, Mwanaidi Athuman Mtanda.

Uteuzi huo umeanza Mei 11, mwaka huu.

Send this to a friend