Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

0
57

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Janet Zebedayo Mbene kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Wakala wa Nishati Vijijini (REA).

Amemteua James Andilile Mwainyekule kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA). Mwainyekule ni Mhasibu Mkuu Tume ya pamoja ya Fedha, Wizara ya Fedha na Mipango, Dodoma.

Rais Samia amemteua Rashid Kassim Mchatta kuwa Skauti Mkuu Tanzania. Mchatta anachukua nafasi ya Mwantumu Mahiza ambaye amemaliza muda wake.

Pia amemteua Gilead John Teri kuwa Mtendaji Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Tanzania (TIC). Teri ni Mshauri Mwandamizi Umoja wa Ulaya (EU), Copenhagen, Denmark.

Amemteua Damasi Joseph Mfugale kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Utalii Tanzania (TTB). Mfugale ni Mshauri Mwandamizi wa Kampuni ya Afrika Chapter EBI International Consulting Group, Canada.

Aidha, Rais Samia amewateua Makamishna wa Tume wawili ambao ni Caroline Joseph Mutahanamilwa kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania, na Idd Ramadhan Mandi kuwa Kamishna wa Tume ya Kurekebisha Sheria Tanzania.

Send this to a friend