Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi mbalimbali

0
60

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Mhandisi Rogatus Hussein Mativila kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – TAMISEMI (Miundombinu). Mhandisi Mativila alikuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Aidha, Rais Samia amemteua Mhandisi Mohamed Besta kuwa Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) ambapo kabla ya uteuzi huo alikuwa ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Wakala wa Usimamizi wa Usalama wa Usafiri wa Anga wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (CASSOA).

Balozi aliyewafananisha Waafrika na nyani arudishwa kwao

Pia amemteua Kamishna Benedict Wakulyamba kuwa Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii akichukua nafasi ya Anderson Mutatembwa ambaye amehamishiwa kuwa Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Bunge na Uratibu).

Amemteua pia Mhandisi Amin Nathaniel Mcharo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS).

Send this to a friend