Rais Samia afanya uteuzi wa viongozi saba

0
72

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya uteuzi kama ifuatavyo:

i) Amemteua Mhandisi Bashir Juma Mrindoko kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Shirika la Utafiti wa Maendeleo ya Viwanda Tanzania (TIRDO). Mhandisi Mrindoko ni Katibu Mkuu Mstaafu.

ii) Amemteua Prof. Shabani Athumani Chamshama kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Misitu Tanzania (TaFF). Prof. Chamshama ni Profesa wa Sayansi ya Misitu na Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA), Morogoro.

iii) Amemteua Bi. Sarah Kinyamfura Barahomoka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Promotion of Rural Initiatives and Development Enterprises Limited (PRIDE). Bi Barahomoka ni Mwandishi Mkuu wa Sheria Mstaafu, Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali.

iv) Amemteua Bw. Paul Thomas Sangawe kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mfuko wa Self Microfinance (Self -MF). Bw. Sangawe ni Mkurugenzi wa Sera na Utaratibu wa Shughuli za Serikali, Ofisi ya Waziri Mkuu, Dodoma.

v) Amemteua Dkt. Oswald Jotam Masebo kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Makumbusho ya Taifa (NMT). Dkt. Masebo ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

vi) Amemteua Prof. Emmanuel Amaniel Mjema kuwa Mwenyekiti wa Baraza la Uongozi la Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM). Prof. Mjema ni Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE), Dar es Salaam.

vii) Amemteua Bi. Tuma Daniel Abdallah kuwa Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN). Bi. Abdallah alikuwa Kaimu Mhariri Mkuu wa Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN).

Send this to a friend