
New Tanzanian President Samia Suluhu Hassan addresses after swearing-in ceremony as the country's first female President after the sudden death of President John Magufuli at statehouse in Dar es Salaam, Tanzania on March 19, 2021. - Hassan, 61, a soft-spoken Muslim woman from the island of Zanzibar, will finish Magufuli's second five-year term, set to run until 2025, after the sudden death of John Magufuli from an illness shrouded in mystery. (Photo by STR / AFP) (Photo by STR/AFP via Getty Images)
Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali kama ifuatavyo:-
• Amemteua Dkt. Florence Martin Turuka kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Kampuni ya Mbolea Tanzania (TFC).
Dkt. Turuka ni Mhadhiri Mwandamizi Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine.
• Amemteua Prof. Sylvia Shayo Temu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taifa ya Uhasibu na Ukaguzi (NBAA).
Prof. Temu alikuwa Mkurugenzi wa Elimu ya Juu (Mstaafu), Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia.
• Amemteua Prof. Ahmed Mohamed Ame kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Takwimu cha Afrika Mashariki (EASTC).
Prof. Ame ni Mhadhiri, Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).
• Amemteua Dkt. Mwamini Madhehebi Tulli kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Chuo cha Uhasibu Arusha (IAA).
Dkt. Tulli ni Mhadhiri Mwandamizi, Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM).
• Amemteua Bw. Jacob Jail Kibona kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Bw. Kibona alikuwa Kaimu Mkurugenzi (Mstaafu), Wakala wa Ugavi na Manunuzi (GPSA).
• Amemteua Dkt. Irene Charles Isaka kuwa Afisa Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Isaka alikuwa Katibu Mtendaji East and Central Africa Social Security Association (ECASSA).
• Amemteua Dkt. Tumaini Katunzi kuwa Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).
Kabla ya uteuzi huo Dkt. Katunzi alikuwa Mkuu wa Chuo Msaidizi, Utawala, Mpango na Fedha, Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).
• Amemteua Bw. Godfrey Basilo Mbanyi kuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Bw. Mbanyi alikuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu, Bodi ya Wataalam ya Ununuzi na Ugavi (PSPTB).
Uteuzi huo umeanza m Novemba 9, 2021.