Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi wafuatao:-
• Amemteua Balozi Ombeni Yohana Sefue, Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Taasisi ya Uongozi (Uongozi Institute). Balozi Sefue anachukua nafasi ya Dkt. Stergomena Tax ambaye ameteuliwa kuwa Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa
Uteuzi huo umeanza tarehe 24 Novemba, 2021.
• Amemteua Balozi Mathias Meinrad Chikawe, Mwenyekiti na Mkurugenzi Mwenza wa Kampuni ya Uwakili ya FMD Legal Consultants and Advocates kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Tanzania International Petroleum Reserves Limited (TIPER).
Uteuzi huo umeanza tarehe 24 Novemba, 2021.
• Amemteua Mhandisi Mussa Ibrahim Iyombe, Katibu Mkuu Mstaafu – TAMISEMI kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Mfuko wa Hifadhi ya Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF).
Uteuzi huo umeanza tarehe 16 Novemba, 2021.
• Amemteua Prof. Ephata Elikana Kaaya kutoka Chuo Kikuu cha Afya na Sayansi Shirikishi Kilimanjaro (KCMUCo), Kilimanjaro kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wadhamini ya Taasisi ya Saratani Ocean Road.
Uteuzi huo umeanza tarehe 15 Novemba, 2021.