Rais Samia ahimiza mahakama kutumia teknolojia kutatua migogoro

0
45

Rais Samia Suluhu Hassan amesema ukuaji wa soko, teknolojia na ubunifu ni moja kati ya mambo ambayo yanaweza kusababisha migogoro na miingiliano, hivyo mahakama ni lazima zijipange kusuluhisha migogogro ya aina hiyo pindi inapotokea.

Ameyasema hayo wakati akishiriki Mkutano Mkuu wa Mwaka na Jukwaa la Majaji Wakuu wa Kusini na Mashariki mwa Afrika Oktoba 23, 2023 mkoani Arusha, ambapo amewataka majaji kutoka nchi 16 za Kusini Mashariki mwa Arika kuzijengea uwezo mahakama katika nchi hizo ili ziwe na uwezo wa kutatua migogogoro kwenye eneo Huru la Biashara Barani Afrika.

“Ninamatumai wakati wa majadiliano yenu katika mkutano huu, mtapata muda wa kuchunguza mfumo mzima wa Eneo la Biashara Huru la Bara la Afrika ili kuuelewa vyema muundo wake,” amesema na kuongeza kuwa “mhimili wa mahakama haukuwa tu na uwezo wa kuhakikisha upatikanaji wa haki kwa wote wanaohitaji, bali pia kuhakikisha usalama wa wafanyakazi wake na watumiaji wa mahakama.”

Rais Samia: Uwekezaji bandarini umezingatia maslahi ya taifa

Aidha, Rais Samia amezungumzia umuhimu wa makama kutumia teknolojia za kisasa katika kusikiliza na kutatua migogoro ya kibiashara inayojitokeza katika eneo hilo.

Mbali na hayo, amesema ubunifu wa teknolojia unahitajika ili kushughulikia masuala yanayohusiana na usalama wa chakula barani Afrika na kukuza biashara na uwekezaji katika upande wa sekta ya kilimo.

Send this to a friend