Rais Samia aifumua MSD, Meja Jenerali Mhidze aondolewa

0
81

Rais Samia Suluhu Hassan amemteua Rosemary William Slaa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Bohari ya Dawa (MSD). Bi. Slaa ni Afisa Mwandamizi katika Kampuni ya PricewaterhouseCoopers (PWC).

Pia amemteua Mavere Ali Tukai kuwa Mtendaji Mkuu wa Bohari ya Dawa (MSD). Bw. Tukai ni Kiongozi Mkuu wa Mradi wa USAID Global Health Supply Chain Technical Assistance.

Tukai anachukua nafasi ya Meja Jenerali Dkt. Gabriel Saul Mhidze ambaye atapangiwa majukumu mengine.

Wakati huo huo, amemteua Raymond William Mndolwa kuwa Mkurugenzi wa Tume ya Taifa ya Umwagiliaji.

Mndolwa ni Mtaalam wa Operesheni, Kampuni ya STC Construction, Dar es Salaam.

Uteuzi wa viongozi hao unaanza mara moja.

Send this to a friend