Rais Samia aifumua TANESCO, atumbua na kuteua wapya

0
42

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi kama ifuatavyo:-

Amemteua Omari Issa kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya TANESCO. Kabla ya uteuzi huo alikuwa Mtendaji Mkuu wa Kitengo cha Ufuatiliaji na Utekelezaji wa Miradi (PDB).

Pili, amemteua Maharage Chande kuwa Mkurugenzi Mkuu wa TANESCO. Kabla ya uteuzi huu, Chande alikuwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kanda ya Afrika Mashariki na Magharibi wa Multichoice Afrika.

Chande anachukua nafasi ya Dkt. Tito Mwinuka.

Tatu, Amemteua Michael Minja kuwa Kamishna wa Petrol na Gesi, Wizara ya Nishati. Kabla ya uteuzi huu Bw. Minja alikuwa mkurugenzi Mkuu – TIPPER.

Nne, amemteua Felschemi Mramba kuwa Kamishna wa Umeme na Nishati Jadidifu. Kabla ya uteuzi huu Bw. Mramba alikuwa Mshauri Mkuu wa Kiufundi (Chief Technical Advisor) – TANESCO Training School.

Tano, amemteua Hassan Seif Said kuwa Mkurugenzi Mkuu, Wakala wa Nishati Vijijini (REA). Kabla ya uteuzi huo alikuwa Meneja wa Kanda Mwandamizi wa Kanda ya Mashariki TANESCO.

Said anachukua nafasi ya Amos Maganga.

Wakati huohuo, Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Hussein Kattanga amewahamisha Watumishi Waandamizi watano toka TANESCO kwenda Ofisi ya Rais, Menejmenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora ambako watapangiwa kazi nyingine kama ifuatavyo:-

1. Mhandisi Khalid James – Naibu Mkurugenzi Mtendaji Uwekezaji.

2. Mhandisi Raymond Seya – Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usambazaji na Masoko.

3. Mhandisi Isaac Chanje – Naibu Mkurugenzi Mtendaji Usafirishaji.

4. Nyelu Mwamaja – Mkuu wa Kitengo cha Ununuzi.

5. Amos Ndegi – Mwanasheria wa TANESCO

Aidha, Waziri wa Nishati, January Makamba amefanya uteuzi wa wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO kama ifuatavyo:

  1. Nehemia Mchechu
  2. Zawadia Nanyaro
  3. Lawrence Mafuru
  4. Mhandisi Cosmas Masawe
  5. Balozi Mwanaidi Maajar
  6. Mhandisi Abdallah Hashim
  7. Abubakar Bakhresa
  8. Christopher Gachuma
Send this to a friend