Rais Samia Suluhu Hassan ametoa zawadi ya shilingi milioni 10 kwa wachezaji wa kikosi cha timu ya Taifa ya wanawake, Twiga Stars, baada ya kuwatoa Ivory Coast katika mchezo wa kuwania kufuzu WAFCON.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Gerson Msigwa amesema Rais Samia amemtuma kuwaeleza kuwa anaunga mkono timu hiyo huku akiwahimiza kujiandaa vizuri kwa ajili ya hatua zinazofuata.
“Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amenituma nije niwaambie anawapenda, anawaunga mkono, hakutangaza hapo kabla lakini leo baada ya matokeo haya atawapa milioni 10. Kwahiyo goli la mama linaendelea na mimi kaka yenu Katibu Mkuu nimekuja kwenye wizara hii hatupoi, lazima kieleweke,” amesema.
Twiga Stars imeibuka na ushindi wa penati 4-2 dhidi ya Ivory Coast na sasa itacheza na mshindi kati ya Togo na Djibouti katika mchezo wa mwisho wa mchujo.
Fainali za WAFCON zitapigwa nchini Morocco mwaka 2024.