Rais Samia aitaka TFF kutenga pesa inazokusanya kukarabati viwanja

0
47

Rais Samia Suluhu Hassan amelitaka Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kuhakikisha linakarabati viwanja vya michezo kwa kutumia pesa wanazokusanya katika michezo na si kusubiri Serikali ifanye hivyo.

Akizunguma leo katika hafla ya chakula cha mchana iliyoambatana na kuipongeza timu ya vijana chini ya umri wa miaka 15, Karume Boys baada ya kutwaa ubingwa wa Kombe la CECAFA nchini Uganda, amesema viwanja vinazalisha fedha, hivyo TFF inapaswa kutenga kiasi kwa ajili ya kufanya marekebisho mapema pindi kunapotekea hitilafu ndogo ndogo.

“Huuo ndio msimamo wangu na ndio nitakaomwambia Rais Mwinyi asimame nao. Viwanja hivi vinajichumia kwa hiyo yale mafungu mnayoyapanga, muweke na fungu la kiwanja,” amesema.

Aidha, ametoa wito kwa wadau mbalimbali wa michezo kuendelea kuiunga mkono Serikali ya pande zote mbili katika juhudi inazofanya za kukuza na kuendeleza michezo nchini Tanzania.

Mbali na hayo amewataka viongozi kubadilika na kujituma ili michezo iendeshwe kwa weledi na kufikia malengo yanayotarajiwa.

Send this to a friend