Rais Samia aitenganisha Wizara ya Afya

0
63

Rais Samia Suluhu Hassan, ameiondoa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii kutoka Wizara ya Afya ili iweze kufanyakazi kwa ufanisi zaidi.

Rais Samia amesema hayo leo tarehe 16 Desemba, 2021 wakati wa uzinduzi wa Kamati ya Ushauri ya Kitaifa ya Utekelezaji wa Ahadi za Nchi kuhusu Kizazi chenye Usawa, Jijini Dodoma.

Amesema Wizara ya Afya ina mambo mengi hivyo ni muhimu kuitenga kwa sababu sekta ya afya peke yake inachukua sura kubwa ya wizara, hivyo ikitenganishwa itafanya kazi zake vizuri na kupitia hilo atamshauri Rais wa Zanzibar naye afanye mabadiliko hayo.

Akizungumza Jukwaa la sasa la Kizazi chenye Usawa, amesema kuwa huo ni mwendelezo wa jitihada mbalimbali zinazofanywa na Umoja wa Mataifa katika kuhakikisha hakuna mtu anayeachwa nyuma kimaendeleo pamoja na kuhakikisha lengo namba 5 la Malengo ya Maendeleo Endelevu (Usawa wa Jinsia na Uwezeshaji wa Wanawake na Wasichana).

Send this to a friend