Rais Samia aja na mbinu mpya kufadhili miradi Serikali za Mitaa

0
25

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Katibu Mtendaji wa Mfuko wa Umoja wa Mataifa wa Mitaji ya Maendeleo (UNCDF), Preeti Sinha, ambaye amemweleza kuwa mfuko huo upo tayari kushirikiana na nchi zinazoendelea ikiwa ni pamoja na Serikali ya Tanzania.

Bi. Sinha amesema ushirikiano huo utajikita katika kuisaidia serikali kutafuta njia mbadala za kupata fedha za kugharamia miradi ya maendeleo, ikiwemo kupitia mradi wao ujulikanao kama Municipal Investment Financing.

Ameeleza kuwa mradi huo utawezesha upatikanaji wa fedha kwa Serikali za mitaa kupitia uanzishwaji wa hati fungani na kwamba fedha zitakazopatikana kupitia Hati Fungani zitarejeshwa kutokana na makusanyo yanayopatikana kwenye Serikali za Mitaa.

Kwa upande wake Rais Samia amekubaliana na wazo hilo na kusema kuwa litasaidia kupunguza mzigo kwa Serikali Kuu kuhudumia miradi ya maendeleo ya Serikali za Mitaa.

Rais Samia ameiagiza Wizara ya Fedha na Mipango kufanya uratibu utakaowezesha mpango huo kuanza kutekelezwa mara moja.

Send this to a friend