Rais Samia ajadili hali ya usalama nchini Msumbiji

0
26

Rais Samia Suluhu Hassan amefanya mazungumzo na Rais wa Baraza la Umoja wa Ulaya (EU), Charles Michel ambaye ambapo lengo ni kupata maoni ya Rais Samia kuhusu mambo manne ya kipaumbele kwa Umoja wa Ulaya kwenye mahusiano yake na Afrika na utayari wa Umoja wa Ulaya kushirikiana na Tanzania kwenye maeneo hayo.

Mambo hayo ni UVIKO 19, mabadiliko ya tabia nchi, hali ya usalama nchini Msumbiji na mapinduzi ya kidijitali.

Kwa upande wake Rais Samia ameushukuru Umoja wa Ulaya kwa ushirikiano wake na kuelezea hatua ambazo Tanzania inachukua katika kukabiliana na UVIKO 19, hasa ikizingatiwa kuwa ugonjwa huo umeathiri sekta nyingi ikiwemo sekta ya utalii.

Pamoja na mambo mengine Rais Samia ameeleza hatua mbalimbali ambazo Serikali inachukua katika kusambaza miundombinu ya afya ingawa bado kuna changamoto katika upatikanaji wa vifaa tiba na rasilimali watu na hivyo kuukaribisha Umoja wa Ulaya kuangalia namna ya kushirikiana na Tanzania katika maeneo hayo.

Kuhusu mabadiliko ya tabia nchi, Mhe. Rais Samia amesema Tanzania ni miongoni mwa nchi zilizoathirika na inalipa kipaumbele suala hilo katika kukabiliana nalo.

Send this to a friend