Rais Samia ajiunga WhatsApp Channel

0
56

Rais Samia Suluhu Hassan ameandika historia nchini Tanzania kwa kuwa kiongozi wa kwanza kutumia na kuthibitishwa kwenye mfumo wa mawasiliano wa WhatsApp Channel, hatua inayomwezesha kufikia umma kwa njia ya kisasa zaidi, sawa na mitandao mingine ya kijamii, na kuwa karibu na wananchi kwa muda wowote.

Mfumo huo wa WhatsApp Channel unamruhusu Rais Samia kuwasiliana na watu wengi zaidi kwa urahisi na kwa haraka, huku akiweza kusikiliza maswali na maoni ya wananchi kwa njia ya moja kwa moja.

Hatua hii inajenga zaidi uhusiano wa karibu kati ya serikali na wananchi, na kuongeza uwazi na ushirikiano kwa kusudi la maendeleo ya nchi.

Rais Samia ahimiza mahakama kutumia teknolojia kutatua migogoro

Mfano wa viongozi mashuhuri wanaotumia huduma hii ni pamoja na Waziri Mkuu wa India, Narendra Modi, ambaye ameonyesha jinsi mfumo huu unavyoweza kuleta mabadiliko chanya katika mawasiliano kati ya serikali na wananchi.