Rais Samia akemea ubabe kwa viongozi wa mikoa na wilaya

0
62

Rais Samia Suluhu Hassan amesema baadhi ya wakuu wa mikoa na wilaya wanatumia vibaya madaraka yao kwa kuendeleza ubabe wakati wa utekelezaji wa majukumu katika maeneo yao, hivyo wanapaswa kujua taratibu za uongozi na mipaka yao.

Akizungumza leo Ikulu Chamwino Jijini Dodoma katika warsha ya kupokea Taarifa ya Kamati ya Kuunda Mkakati wa Utekelezaji wa Mapendekezo ya Tume ya Haki Jinai, amesema viongozi wote haijalishi nafasi zao wanapaswa kuzingatia taratibu za kazi kwani kila kazi ina mipaka yake.

“Waraka namba 1 wa mwaka 2023 wa Katibu Mkuu Kiongozi kwa Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya unaoelekeza na kusisitiza uzingatiaji wa sheria na kanuni katika utekelezaji wa mamlaka yao ya ukamataji uende ukatekelezwe vema, pamoja na waraka ule ambao umetolewa mwaka jana, bado kuna wakuu wa mikoa na wakuu wa wilaya wanaendeleza ubabe kule maeneo walipo,” amesema.

Aidha, amesema wajibu wa kuimarisha haki za raia kama zilivyoelezwa kwenye katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, si suala la hiari isipokuwa ni suala la kuifanyia kazi ipasvyo ili kila mmoja apate haki anayostahili.

Send this to a friend