Rais Samia akemea uvujifu wa taarifa za Serikali mitandaoni

0
46

Rais Samia Suluhu Hassan amekemea tabia ya baadhi ya watunza kumbukumbu kuvujisha taarifa za Serikali kwenye mitandao ya kijamii kwa maslahi yao binafsi.

Amesema hayo leo Novemba 27, 2022 wakati alipokuwa akishiriki ufunguzi wa mkutano wa 10 wa Chama cha Taaluma ya Menejimenti ya Kumbukumbu Tanzania (TRAMPA) jijini Arusha.

“Kuna mambo tunayaonaona huko kwenye mitandao, kumbukumbu za Serikali ziko huko kwenye mitandao […] sasa unajiuliza huyu aliyetoa hizi taarifa anataka umaarufu, rushwa au kitu gani?” amehoji Rais Samia.

Aidha, amesisitiza chama kuwa na namna nzuri ya kujadili na kutatua changamoto kwa utaratibu sahihi wa majadiliano na mamlaka zilizopo, huku akiahidi kuwasikiliza changamoto zao na kuwalinda kwa hali zote kwakuwa ndio kitovu cha kazi zote za Serikali.

Send this to a friend