Rais Samia akemea viongozi kujimilikisha vyama vya siasa

0
65

Rais Samia Suluhu Hassan ametoa wito kwa vyama vya siasa kujijadili na kujitathmini wao wenyewe kuhusu mienendo yao ndani ya vyama kwa kuwa ni mijadala yenye afya kwa taifa.

Ameyasema hayo leo Oktoba 21, 2022 Ikulu jijijni Dar es Salaam wakati akipokea Ripoti ya Kikosi Kazi cha Kuratibu maoni ya wadau wa demokrasia ya vyama vingi vya siasa iliyowasilishwa na Mwenyekiti wa Kikosi Kazi, Profesa Rwekaza Mukandala.

“Kila mwaka siku ambayo kikosi kimependekeza kaeni mjijadili, na msijadili tu Serikali inavyoendesha shughuli za siasa, lakini wakati wa kujijadili na nyinyi wenyewe, nani anafanya nini, tunakwenda vipi kwenye siasa zetu, tunakosea wapi, wapi tumetia chumvi, wapi tumepazimua, ni mijadala yenye afya,” amesema Rais Samia.

Rais Samia ataka wananchi kupewa elimu ya sheria zinazotungwa

Baadhi ya mapendekezo yaliyotolewa na Kikosi Kazi hicho ni pamoja na Tume ya Taifa ya Uchaguzi kutolazimika kufuata amri au maagizo ya mtu, idara au taasisi yoyote, mikutano ya hadhara na mikutano ya ndani ya vyama vya siasa kuendelea kwa mujibu wa Katiba pamoja na asilimia 10 ya fedha za ruzuku kwa vyama vya siasa zinazotengwa katika bajeti ya Serikali kugawiwa sawa kwa vyama vyote vya siasa vyenye usajili kamili.

Hata hivyo, Rais Samia amewapongeza wote walioshiriki katika Kikosi Kazi na kuahidi kuyapa kipaumbele zaidi yale ambayo yataleta athari kubwa kwa jamii, na kwa yale ambayo yatahitaji gharama kubwa yatatekelezwa kuendana na hali ya mfuko wa Serikali kiuchumi.

Send this to a friend