Rais Samia akemea vyama vya ushirika vinavyowakandamiza wakulima

0
26

Rais Samia Suluhu Hassan amevitaka vyama vya ushirika kuwalinda, kuwasimamia na kuwatetea wanaushirika na sio kuwanyonya na kuwakandamiza kwa manufaa yao binafsi.

Akizungumza katika kikao na Maafisa Ugani na Maafisa Ushirika Ikulu mkoani Dodoma, amesema baadhi ya viongozi wa vyama vya ushirika wamekuwa wakiwadhulumu wakulima katika mauzo ya mazao na kurudisha nyuma maendeleo ya wanaushirika.

“Ni lazima vyama vya ushirika vie mstari wa mbele kumlinda na kumtetea mwanamshirika badala ya kuwa wa kwanza kumnyonya na kumkandamiza” amesema.

Aidha, amesema Afrika ndilo bara linalotegemewa kuzalisha chakula kwa ajili ya kuilisha dunia kutokana na hali ya kutokuwepo kwa usalama wa chakula duniani, hivyo Tanzania ina kila sababu ya kukimbilia fursa hiyo.

“Dunia hii inakumbwa na kutokuwa na usalama wa chakula, lakini Afrika ndilo bara linalotegemewa kuzalisha chakula. Ukichukua Afrika, Tanzania sisi hatuna sababu ya kuwa nyuma kwenye uzalishaji wa chakula, kuilisha Afrika na kuilisha dunia,” ameeleza.

Mbali na hayo, amevitaka vyama vya ushirika kuwahamasisha wanaushirika kuwa na bima za afya ili ziwasaidie hasa wanapokuwa wazee ili kuondoa mzigo kwa Serikali.

Send this to a friend