Rais Samia akutana na mjumbe wa Waziri Mkuu wa Uingereza

0
31

Rais Samia Suluhu Hassan amekutana na kuzungumza na Mjumbe Maalum wa Waziri Mkuu wa Uingereza, Boris Johnson, kuhusu masuala ya biashara kati ya Uingereza na Tanzania, Lord Walney.

Viongozi hao wamejadili fursa mbalimbali za biashara na uwekezaji nchini ikiwa ni pamoja ufanisi katika kuvutia wawekezaji kutoka nchini Uingereza na wafanyabiashara wa Tanzania kuuza bidhaa zao nchini Uingereza.

Rais Samia amesema Serikali ya Tanzania itaendelea kushirikiana na Serikali ya Uingereza katika kuchochea biashara baina ya nchi mbili hizo.

Wakati huohuo, Rais Samia amekutana na kuzungumza na Mwenyekiti wa Mabenki ya United Bank for Africa (UBA), Dkt. Tony Elumelu kuhusu nyanja mbalimbali za operesheni ya benki hiyo hapa nchini.

Dkt. Elumelu amemhakikishia Rais Samia utayari wa benki hiyo katika kutatua changamoto mbalimbali za kiuchumi ikiwemo ufadhili wa miradi ya mafuta na gesi.

Kwa upande wake,Rais Samia amemueleza Dkt. Elumelu kuwa Serikali ya Awamu ya Sita iko tayari kufanya kazi na benki hiyo hivyo kumkaribisha kuwekeza kwenye miradi husika.

Send this to a friend