Rais Samia alifumua Shirika la Posta

0
25

Rais Samia Suluhu Hassan ametengua uteuzi wa viongozi watatu wa Shirika la Posta Tanzania
kuanzia Aprili 30, 2021.

Kwanza, ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Shirika la Wakala wa Meli Tanzania (TASAC) Prof. Tadeo Andrew Satta.

Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia pia ametengua uteuzi wa wajumbe sita wa bodi ya TASAC.

Pili, ametengua uteuzi wa Posta Masta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania, Hassan Mwang’ombe.

Tatu, Rais Samia ametengua uteuzi wa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania Dkt. Harun Kondo.

Sambamba na hatua hiyo, Rais Samia pia amevunja Bodi ya Wakurugenzi wa Shirika la Posta Tanzania.

Uteuzi wa viongozi watakaoshika nyadhifa hizo utafanywa baadaye.

Send this to a friend