Rais Samia amefanya uteuzi na uhamisho kwa baadhi ya viongozi

0
41

Rais Samia Suluhu Hassan amemhamisha David Silinde kuwa Naibu Waziri wa Kilimo akichukua nafasi ya Antony Mavunde ambaye ameteuliwa kuwa Naibu Wazi wa Madini.

Pia, amemteua mbunge wa Misungwi, Alexander Mnyeti kuwa Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi akichukua nafasi ya Antony Silinde.

Rais Samia amemteua Balozi Mhandisi Aisha Amour kuwa Katibu Mkuu Wizara ya Ujenzi.

Aidha, Rais amewateua wajumbe wanne wa tume ya mipango akiwemo Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu, Balozi Ombeni Sefue, Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TANESCO, Omary Issa, Balozi Mstaafu, Ami Mpungwe pamoja na Meneja Mkazi wa Benki ya Dunia nchini Cambodia, Mariam Salim.

Send this to a friend