Rais Samia amlilia Mzee Kaunda

0
50

Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan ameeleza kusikitishwa na kifo cha mwasisi na Rais wa kwanza wa Zambia, Kenneth Kaunda kilichotokea leo.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Rais Samia ametoa pole kwa Rais wa Zambia, Edger Lungu, wanafamilia ya Kaunda na raia wa Zambia kwa kuondokewa na mwanamajumui huyo aliyepigania ukombozi wa Afrika.

“Nimesikitishwa na kifo cha Mzee wetu Kenneth Kaunda, Rais Mstaafu wa Kwanza wa Zambia. Afrika tumeondokewa na mpigania ukombozi, mzalendo na mwanamajumui wa kweli. Nakupa pole kaka yangu @EdgarCLungu wana familia na Wazambia wote. Mungu amweke mahali pema Mzee KK, Amina,” ameeleza Rais Samia.

Rais Kaunda amefariki akiwa na umri wa miaka 97, ikiwa ni siku tatu tangu alipofikishwa hospitalini mjini Lusaka.

Kaunda aliiongoza Zambia kwa miaka 27 kuanzia 1964 hadi 1991, akiwa ni Rais wa kwanza wa Zambia huru. Aliongoza mapambano dhidi ya utawala wa kikoloni katika nchi nyingine za Kusini mwa Afrika, ikiwemo Afrika Kusini.

Send this to a friend