Rais Samia amteua Rais Kikwete kwa muhula wa pili

0
67

Rais Samia Suluhu Hassan, amefanya uteuzi wa viongozi mbalimbali;

1. Amemteua Rais Mstaafu, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Chancellor) kwa kipindi kingine cha miaka sita (06) kuanzia tarehe 17 Januari, 2022.

2. Amemteua Balozi Ramadhani Muombwa Mwinyi kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Diplomasia (CFR).

Balozi Mwinyi ni Naibu Katibu Mkuu Mstaafu wa Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki.

3. Amemteua Balozi Begium Kaim Taji kuwa Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Arusha International Conference Centre (AICC). Balozi Taji ni Balozi Mstaafu wa Tanzania, Paris nchini Ufaransa

Teuzi hizi zimeanza Desemba 28, 2021.

4. Amemteua Patience Kilanga Ntwina kuwa Katibu Mtendaji wa Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora.

Ntwina alikuwa Mkurugenzi, Idara ya Katiba na ufuatiliaji wa Haki kutoka Wizara ya Katiba na Sheria.

Uteuzi huu umeanza Desemba 30, 2021.

Send this to a friend