Rais Samia: Anayetoa chakula nje ya nchi awe na kibali cha Wizara ya Kilimo

0
28

Rais Samia ametilia mkazo kwa wananchi kutosafirisha mahindi nje ya nchi bila vibali vya Wizara ya Kilimo na taratibu nyingine zinazotakiwa kwa kuwa zinaathiri uchumi na soko la kibiashara.

Ameyasema hayo wakati wa uzinduzi wa vihenge na maghala ya kisasa ya Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula (NFRA), katika eneo la Kanondo, Mkoani Rukwa ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake mkoani humo.

“Tunajenga vihenge na maghala ili wakulima mnapovuna basi tuweze kununua serikali na kuhifadhi kwa haraka. Mnapofungua vinjia vya ajabu ajabu huko na kupakia kwenye magari chakula kiende nje bure Serikali hatupati kitu. Niwaombe sana Mkuu wa Mkoa fuatilia hilo lakini wakuu wa wilaya kuhakikisha chakula hakitoki, anayetoa chakula nje awe na kibali kutoka Wizara ya Kilimo,” amesema.

Aidha, Rais Samia ameelekeza mbolea za ruzuku ziendelee kuwepo pamoja na kusisitiza mahindi yanunuliwe kutoka kwa wakulima wa vijijini kwa gharama ya shilingi 600 kwa kilo na mjini shilingi 650 kwa kilo.

Mbali na hilo, ameelekeza mizani ya kidigitali iongezwe kwa wingi katika vituo vya NFRA ili kurahisisha huduma kwa wakulima kwa kupata haki stahiki ya uzito wa mazao yao.

Send this to a friend