Rais Samia aomboleza vifo vya watu 10 Kisiwani Pemba

0
59

Rais Samia Suluhu Hassan ametuma salamu za rambirambi kwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi kufuatia vifo vya watu 10 katika ajali boti.

Ajali hiyo imetokea Januari 4, 2022 katika eneo la bahari ya Kisiwa Panza, Wilaya ya Mkoani, Mkoa wa Kusini Pemba, Zanzibar.

Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Kusini Pemba, Richard Mchomvu, watu hao walikuwa wanatoka Chakechake kuelekea kwenye mazishi katika Kisiwa Panza.

Rais Samia amemuomba Rais Dkt. Mwinyi kufikisha salamu zake za pole kwa wafiwa wote, ndugu, jamaa pamoja na marafiki na anaungana na familia hizo katika kipindi hiki kigumu cha majonzi.

Rais Samia pia amewaombea kwa Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu mahali pema peponi, Amina.

Send this to a friend