Rais Samia apandisha dau hadi milioni 20 kwa kila goli kwa Yanga

0
45

Rais Samia Suluhu Hassan ametangaza kuongeza fedha za motisha kwa timu ya Yanga kutoka TZS milioni 10 hadi TZS milioni 20 kwa kila goli la ushindi katika michezo ya fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika.

Pia ametoa ndege itakayowapeleka na kuwarudisha wachezaji wa klabu ya Yanga pamoja na mashabiki katika mchezo huo nchini Algeria kwenye mchezo wao dhidi ya USM Alger.

Rais Samia ametoa ahadi hiyo leo Mei 18, 2023 katika hafla ya uzinduzi wa minara 21 ya kurushia matangazo ya televisheni ardhini (DTT) ya kampuni ya Azam Media Ltd jijini Dar es Salaam.

Serikali yapeleka mashabiki 55 wa Yanga Afrika Kusini

“Naomba sana wale viongozi wa TFF kuwapa moyo kama Serikali tunavyofanya kuwapa moyo, kuwasemea vizuri ili tuwape hamasa waende wakamalize mchezo huu vizuri sana,” amesema

Rais Samia alianza na ahadi ya TZS milioni tano kwa kila goli kwa timu ya Simba na Yanga katika michezo ya kimataifa ya Afrika na baadaye kupandisha dau  hadi milioni 10 katika mchezo wa nusu fainali ambapo klabu ya Simba haikufanikiwa kuingia nusu fainali.

Send this to a friend