Rais Samia apongezwa kwa kukuza sekta ya michezo

0
31

Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezao imempongeza Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuwa mstari wa mbele katika kuunga mkono michezo na kuwa kichocheo kikubwa cha ukuaji wa sekta hiyo.

Ameyasema hayo leo Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Balozi Dkt. Pindi Chana wakati akiwasilisha bajeti ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2023/24 bungeni jijini Dodoma.

“Mchango wa Mheshimiwa Rais ndiyo chachu ya mafanikio ya timu za Simba na Yanga katika mashindano haya na kuiwezesha kufikia fainali kwa timu ya Yanga,” amesema Waziri.

Ameongeza “kama ambavyo Waswahili husema mwana hutazama uchogo wa mamaye, timu zinamwahidi kuendelea kuongeza jitihada. Hakika huyu ndiye mwanamichezo wa kweli na wa vitendo siyo wa maneno tu.”

Aidha, Wizara imempongeza Rais Samia kwa mafanikio makubwa yaliyopatikana ndani ya kipindi cha miaka miwili katika sekta hiyo ambayo yametokana na uongozi wake mahiri, pamoja na kuahidi kumpa ushirikiano ili kufanikisha azma yake.

Send this to a friend