Rais Samia asema Royal Tour imetoa fursa za kibiashara kwa wanawake

0
34

Rais Samia Suluhu Hassan amesema filamu ya Royal Tour imesaidia kutoa fursa za biashara kwa wanawake wajasiriamali na kuwawezesha kujiinua kiuchumi, hivyo wametakiwa kutumia fursa hiyo kuzalisha bidhaa bora zaidi.

Amesema hayo leo wakati wa kilele cha maadhimisho ya miaka 25 (Silver Jubilee) ya mfuko wa Fursa sawa kwa wote (EOTF) iliyofanyika katika ukumbi wa JNICC jijini Dar es salaam.

Aidha, amesema Serikali itaendelea kushirikiana na mashirika binafsi pamoja na taasisi za kidini kutoa huduma pamoja na kuchangia maendeleo ya jamii hasa kwa wananchi wanaoishi katika mazingira duni.

Mbali na hayo amewataka wazazi kuacha kuwatelekeza watoto kwakuwa tabia hiyo inazalisha taifa lenye wananchi wasio madhubuti.

Send this to a friend