Rais Samia asema Tanzania imepiga hatua usawa wa kijinsia

0
17

Rais Samia Suluhu Hassan amesema Tanzania imejitahidi kupiga hatua katika usawa wa kijinsia kwa kutoa fursa mbalimbali kwa wanawake hasa katika nafasi za uongozi za kimkakati.

Ameyasema hayo katika Mkutano wa 42 wa SADC uliofanyika nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC).

Aidha, amesisitiza umuhimu wa usalama wa chakula katika ukanda mzima wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) na kuzisihi nchi hizo kuwekeza kwenye ‘Uchumi wa Buluu.’

Bashungwa:Serikali itawashughulikia watumishi wanaodhani zama za upigaji zimerudi

Hata hivyo, Rais Samia ametoa maoni yake kwa lugha ya Kiswahili katika mkutano huo ikiwa ni jitihada za kukuza matumizi ya lugha hiyo miongoni mwa nchi za SADC pamoja na kusisitiza uharakishwaji wa mchakato wa Kiswahili kupitishwa rasmi kama lugha ya nne ya Jumuiya ya SADC.

Rais Samia anategemea kufanya ziara yake ya kikazi ya siku moja nchini DRC ambapo pamoja pia atafanya mazungumzo na mwenyekiti wake, Rais Felix Tshisekedi.

Send this to a friend