Rais Samia asema usasa unawaharibu vijana

0
43

Kutokana na takwimu za Sensa iliyofanyika mwaka 2022 kuonesha kuwa idadi ya vijana ni kubwa zaidi nchini, Rais Samia Suluhu Hassan amewapa jukumu machifu wenzake kuwa walezi wa vijana ili maadili ya taifa yasiharibiwe.

Akizungumza katika Tamasha la Utamaduni wa Bulabo lililofanyika katika uwanja wa Redcross Ngomeni Kisesa mkoani Mwanza, Rais Samia amesema vijana wasipopata usimamizi madhubuti taifa litapotea.

“Vijana hawa wanataka kulelewa, vijana wanataka kuelekezwa, vijana wanataka kuoneshwa njia. Tukiwaacha waende wanavyokwenda na usasa taifa limeharibikiwa,” amesema.

Ameongeza “Usasa ndio lakini usasa wa aina gani, warudisheni nyuma wajitambue watambue mila na desturi zao wakilinganisha na usasa uliopo.”

Mjema: Rais Samia aachwe afanye kazi alete maendeleo

Aidha, ametoa wito kwa Sekta ya Utamaduni kuangalia na kuipa kipaumbele utalii wa utamaduni wa taifa kwa kuendeleza matamasha mbalimbali ili mataifa mengine yaweze kuvutiwa zaidi na nchi kujipatia mapato.

Katika hotuba hiyo, Rais Samia amewataka viongozi hao kuwa mstari wa mbele katika kuzielimisha jamii dhidi ya imani potofu ambazo zimekuwa zikigharimu maisha ya Watanzania wengine pamoja na kuendelea kuliombea taifa.

“Jukumu hili linaweza kufanywa vizuri na machifu kwa sababu Watanzania sote imani yetu ipo kwa machifu, wanapokuja kwetu machifu, hawaji na imani za kisiasa, wanakuja na imani zetu za kijamii,” ameeleza.

Send this to a friend