Rais Samia ashinda tuzo ya Rais wa Dhahabu

0
38

Rais Samia Suluhu Hassan ametangazwa na Jumuiya ya Kimataifa ya Watetezi na Amani kuwa mshindi wa tuzo mbili za kimataifa ikiwemo ya amani duniani 2022 na tuzo ya Rais wa Dhahabu ya Malengo ya Maendeleo Endelevu.

Akizungumza Mwenyekiti wa Taifa wa Umoja wa Wanawake wa CCM (UWT), Gaudencia Kabaka amesema miongoni mwa mambo yaliyomfanya Rais Samia kupata tuzo hizo ni uboreshaji wa miundombinu ya afya na elimu ndani ya kipindi kifupi cha uongozi, utetezi wa masuala ya amani ikiwemo uhuru wa kuabudu na amani.

Mengine ni kujali masuala ya kijinsia kwa kuteua wanawake wengi katika uongozi, ujenzi wa madarasa katika shule za sekondari na msingi na utoaji wa elimu bila malipo.

Aidha, Kabaka amesema Rais Samia alitangazwa kuwa mshindi wa tuzo hizo wiki iliyopita, na atakabidhiwa tuzo hiyo Oktoba 24, mwaka huu.

Marais waliowahi kupata tuzo hizo ambazo Rais Samia atakabidhiwa kwa Afrika ni Rais wa Liberia, George Weah na Rais wa Botswana, Ian Tseretse Khama.

Send this to a friend