Rais Samia asisitiza JWTZ kuendelea kuwa Jeshi la mfano Afrika

0
26

Rais na Amiri Jeshi Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi na Usalama, Samia Suluhu Hassan amelitaka Jeshi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) kuendelea kulinda misingi ya kuanzishwa kwa jeshi hilo na kuendelea kudumisha nidhamu, utii, uaminifu na uhodari uliopo katika jeshi hilo.

Ameyasema hayo wakati akifunga zoezi la Medani katika kuadhimisha Miaka 60 ya JWTZ katika eneo la Pongwe Msungura, lililopo Msata.

Aidha, Rais Samia amesisitiza JWTZ kuendelea kuwa Jeshi la Wananchi la ukombozi la mfano kwa Afrika na dunia kwa namna linavyoonesha uhodari, weledi na nidhamu ya kijeshi.

Ameongeza kuwa jeshi imara zaidi litatokana na dhamira ya kweli, moyo wa kujituma na uchumi imara zaidi.